Zidane Anamtaka Mane kwenye Kikosi Chake

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedin Zidane amesema anamtaka mchezaji wa Liverpool raia wa Senegal Sadio Mane kwenye kikosi chake.

Mane ambaye ameonyesha mchezo mzuri msimu huu akifunga mabao 11 tangu mwaka ianze , huko akifunga mabao saba kwa mechi tano zilizopita na pia kufunga mabao za kimataifa dhidi ya Watford kwenye ligi kuu ya Uingereza na Bayern Munich kwenye kombe la klabu bora Eufa.

Tangu kocha huyo Mfaransa kurejea Santiago Bernabeu Mane amekuwa akitarajiwa kuungana na timu hiyo kwa kuwa Zidan alikuwa akimtaka sana kabla kujiuzulu msimu uliopita.

Mane mwenye umri wa miaka 26 hajaonyesha hisia yeyote ya kujiunga na Madrid.

Guillem Balague ambaye ni mtaalam wa soka uhispania amesema kwamba hakuna uwezekano ya Mane kuja Madrid msimu huu.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals