Marufuku Kwa Mifuko Sokoni

Hisia mbalimbali zinazidi kutolewa na wananchi kuhusu agizo ya serekali kupitia mamlaka ya utunzi 
wa Mazingira NEMA ili kupiga marufuku mifuko vya kubeba bidhaa sokoni almaarufu Uhuru bag.
 
NEMA inadai kuwa mifuko hizo hazijatimiza kiwango inayotakikana na shirika la kugadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS.

Mifuko hizo hazifai kuwa kwenye maduka na soko kuanzia jumapili tarehe 31 mwezi huu.Hivyo basi atakaye patikana nayo atakuwa anakiuka sheria na uhenda akafungwa.

Nilipozungumza na baadhi ya wakazi wa Kisumu kwenye soko la Kibuye wamesema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la serikali ,kwa sababu watakosa mifuko vya kuwahekea wateja wao  bidhaa wanaponunua kutoka kwao.

Vile vile waliomba serikali ya kaunti kutengeneza vituo vya kutupa taka ili kupunguza uchafuzi wa mazingira kwenye soko zao

Comments

Popular posts from this blog

Nigeria win 10th WAFCON as comeback stuns Morocco

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!