Yaliyotekea Kwenye Ligi Kuu Uingereza


Timu ya Chelsea wameongeza matumaini yao ya kumaliza ligi ligi kuu ya Uingereza kwenye nne bora,hii ni baada ya kutoka nyuma bao moja na kushinda Cardif City kwa mabao mawili kwa moja siku ya jumapili ugani Cardif.

Cardif City walipata bao mnamo dakika ya 46  mguu yake Víctor Camarasa lakini Chelsea walijibu bao hiyo kipindi cha pili mnamo dakika ya 84 kupitia kwa nahodha yao Cezar Azpilicueta  kabla ya Rouben Loftus Cheek kuingizwa dakika za ushee na kufunga bao la ushindi kutoka kwa krosi yake Wilian.

Mchezaji bingwa raia wa Ubelgiji Eden Hazard alileta matumaini kwa timu ya Chelsea alipoingizwa baada ya timu hiyo kushindwa kupata bao.

Ushindi huo imempea Meneja Maurizio Sarri afueni baada ya mashabiki kutaka afutwe kazi .

Matokea hiyo pia ina maana kuwa chelsea wako kwenye nafasi ya tano  wakitoshana na Arsenal na pointi 60,huko wakiwa pointi moja nyuma ya Manchester United.

Meneja wa Cardif Warnock hakufuraishwa na maamuzi ya bao la Azpilicueta huko akidai mchezaji huyo alikuwa ameotea akifunga bao .Walitupiana maneno na kocha wa chelsea baada ya mechi hiyo kuisha.

Kwingineko,Liverpool walishinda Totenham kwa mabao mawili kwa moja ugani Anfield na kusonga hadi nafasi ya kwanza kwenye ligi kuu Uingereza.

Makosa ya Mlinda Langu Hugo Lloris ilisaidia Liverpool kupata ushindi walioitaji ili kupita viongozi wa ligi Manchester City.

Roberto Firmino alitangulia kufunga dakika ya kumi na sita tu ya mchezo lakini vijana wa Klopp walisawazisha bao hilo mnamo dakika ya 70 kupitia kwa mchezaji wao Lucas Moura.

Mechi hiyo ilikuwa karibu kutoka sare ya bao moja kwa moja kabla ya Toby Alderweireld kujifunga mnamo dakika ya 90 kutokana na makosa yake mlinda lango Lloris.



Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals