Ombi la Kogalo lakataliwa!
Shirikisho la soka nchini KPL imekataa ombi la Gor mahia ya
kuairisha mechi yao dhidi ya kakamega homboyz inayopaswa kuchezwa siku
ya alhamisi.
Kogalo wameomba kutoshirikishwa
kwenye mechi hiyo ya ligi ili kuwapa muda wa kutosha ya kujitayarisha
kwa mechi yao ya mwisho kwenye kikundi cha D kwenye
kombe la Caf Confederation.
Gor mahia
walipoteza dhidi ya Zamalek nchini Egypt kwa mabao nne kwa sufuri hivyo basi ni lazima washinde
mechi yao ya mwisho dhidi ya Petro Atletico siku ya jumapili.
Kocha
wa Gor mahia Hassan Oktay amesema kuwa wachezaji wake wanahitaji kuenda
kwenye mechi hiyo wakiwa asilimia 100 ili kuhakikisha wameshinda na
kujipea nafasi kwenye robo fainali.
Comments
Post a Comment