Mgomo Ya Wafanya Kazi Wa Ndege

Hii ni baada ya waziri wa uchukuzi James Macharia, kutangaza kuwa mgomo huo ni haramu baada ya wafanyakazi walio chini ya Muungano wa Wafanyikazi wa Viwanja vya ndege nchini – KAWU kugoma, licha ya kuwepo agizo la mahakama kuzuia mgomo huo.
Awali, Katibu Mkuu wa Muungano wa KAWU Moses Ndiema, alikamatwa. Ndiema alikamatwa saa chache baada ya wanachama wa Muungano huo, kuanza mgomo leo asubuhi.
Mgomo huo umesababisha Maelfu ya Wasafiri kukwama katika viwanja vikuu vya ndege nchini, ikiwemo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu na Uwanja wa Ndege jijini Mombasa.
Hata hivyo, hali haijaimarika kwenye viwanja vya Ndege vya Kisumu na Mombasa .
Comments
Post a Comment