Mahakamani
Mwanamme
mmoja kwa jina Brian Opiyo Okumu, ameshtakiwa kwenye mahakama ya Winam jijini
Kisumu kwa kosa la kuiba ng'ombe.
Mbele
ya
hakimu Jackline Mitei, mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa alimwibia
Richard Ajango ng'ombe mwenye dhamana ya shilling alfu 45 mnamo tarehe 4
mwezi huu, eneo ya Koluwa kaunti ya kisumu .
Mshtakiwa
alikanusha mashtaka, na kuomba kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa
kwa dhamana ya shilingi alfu 25 pesa taslimu, au shilingi alfu 50 na mdhamini
wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo
itasikilizwa tarehe 4 mwezi Juni, mwaka huu
Comments
Post a Comment