Mashetani Wekundu Washambuliwa Na Wenye Bunduki

Timu ya Arsenali walicharaza Manchester united kwa mabao mawili kwa sifuri ugani emirates siku ya jumapili usiku kwenye mechi ya kung'ang'ania taji la EPL.

Arsenali walionyesha mchezo nzuri sana kwenye mechi hiyo na kuwazima vijana wa Ole Gunner kama mishumaa.

Wenye bunduki,ukipenda Arsenal walipata bao lao la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Mswiz Granit Xhaka mnamo dakika ya kumi na mbili kabla ya Mgabon Pierre Emerick Aubameyang kuongeza la pili mnamo dakika ya sitini ta tisa kupitia mkwaju wa penalti.

Arsenali walimiliki mpira kwa asilimia 54 na za mchezo huko manchester wakiiguza mpira kwa asilimia 46.

Manchester united hawakuweza kutumia nafasi zao vizuri kwa hivyo walilia chooni baada ya mechi kuisha  kwa kushindwa kwa mabao mawili.

Ushindi huo imepandisha Arsenali hadi nafasi ya nne kwenye jedwali ya ligi kuu uingereza wakiwa na pointi 63,pointi tano mbele ya manchester ambao wako nafasi ya tano.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals