Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!
Klabu ya Gor Mahia almaarufu kama Kogalo wamekuwa timu ya kwanza nchini kufuzu kwenye robo fainali kwenye mashindano ya kung'ang'ania taji la klabu bingwa Afrika .
Kogalo walibaki watu tisa kwenye mechi hiyo baada ya wachezaji wao Ernest Wendo na Shafiq Batambuzi kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi hiyo iliyochezwa ugani kasarani mnamo jumapili.
Gor mahia walionyesha umahiri wao kwenye mechi hiyo na kulazimisha timu ya petro Atletico kuenda nyumbani na kubanduliwa kutoka kwa mashindano hayo.
Kumbuka Kogalo walihitaji ushindi wowote kwenye mechi hiyo ilinkufuzu huko Petro Atletico wakitaka tu sare yeyote ile .Kwa hivyo ilikuwa mechi ya kukata na shoka huko kila timu ikijaribu kujipea tiketi kwenye robo fainali lakini mwishowe Kogalo ndio waliotoka na ushindi .
Kogalo walipata bao yao mnamo dakika ya 56 kupitia mchezaji Jacquis Tuyisenge na mkwaju wa penalti .
Kocha wa Kogalo Hassan Oktay alionyeshwa kadi nyekundu na kufukuzwa kando ya uwanja baada ya kukosana na waamuzi wa mechi hiyo hivyo basi kuacha kocha msaidizi Zedekiah 'Zico' Otieno kupeana mawaidha kwa wanakogalo.
Mashabiki walifurika furifuri kushangilia ushindi huo wa kogalo na hata kujibwaga uwanjani huko wakiimba na kushangilia kwa nduru na vigelegele.
Kongole Kogalo.

Comments
Post a Comment