Makazi Bora

Nyumba na makazi bora ni mojawapo ya agenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, wakenya wengi wangali wanaishi kwenye nyumba duni, zilizo kwenye mazingira chafu, bila maji, ukosefu wa vituo vya afya na usalama duni.

Nilitembelea mtaa wa Bandani jijini Kisumu, na kushuhudia baadhi ya nyumba ambazo hali zao si nzuri kwa binadamu yeyote yule kuishi.

Baadhi ya nyumba hizo hazina vyoo, huku wakaazi wakiishi kwenye nyumba hizo kwa sababu ya mapato duni.
Insert…………..wakaazi………………

Hata hivyo, wakaazi wa Bandani kwa sasa wanaendelea na juhudi za kufanikisha ujenzi wa nyumba bora mtaani humo.

Kupitia Project Management Committee – PMC, wakaazi wa eneo hilo wanaundaa matofali ya kuwawezesha kujenga makaazi bora siku za usoni.

Abubakar Hassan Makengeza ni Mwenyekiti wa PMC.
Insert…………………abubakar………….

Chini ya mpango wa uimarishaji,serikali ya kaunti ya kisumu-CIDP makazi bora ni mojwapo ya malengo yaliyoainishwa.

Serikali hiyo ikitazamia kuhakikisha wakazi wanaishi katika nyumba bora na sio bora nyumba. 
Kemah Amayo-Tunguu ya radio sahara,Kisumu.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals