Pigo Kwa Manchester United
Mchezaji wa Manchester united Alexis Sanchez anahofiwa kuwa nje kwa mwezi miwili kwa kupata majeraha.
Mchile
huyo alipata majeraha kwa magoti kwenye mechi yao dhidi ya Southhampton
siku ya Jumamosi na kulazimishwa kutoka nje baada ya dakika 52 tu za
mchezo.
Sanchez atakosa mechi ya marudiano dhidi ya PSG kwenye kombe la kung'ang'ania bingwa la taji ya Europa EUFA kabla kukosa dhidi ya Arsenal na Wolves .
Mchezaji huyo wa kati ameianzia Manchester united kwenye kumi na moja bora mara nane huko akifunga bao moja.
Sanchez mwenye umri wa miaka 30 amekuwa na wakati ngumu tangu kuungana na Manchester United mwezi wa Januari mwaka jana.
Alexis amefunga mabao tano tu kwa mechi 40 alizochezea Manchester.
Comments
Post a Comment