Manchester Na Kibarua
Timu ya Manchester United leo usiku wako na kibarua kubwa dhidi ya vijana wa PSG ugani Parc des Princes.
Manchester
walishindwa kwenye mechi ya mkondo wa kwanza kwao Old Traford kwa
mabao mawili kwa sufuri kwa hivyo ni lazima wapate ushindi wa mabao
matatu kwa sufuri ili kujipea nafasi kwenye robo fainali ya kombe hilo
la Eufa.
Manchester United watakosa huduma za
wachezaji wao Paul Pogba ambaye anahudumia marufuku baada ya kuwa na
kadi nyingi za njano pamoja na Anthony Martial na Anthony Valencia
ambao wako na majeraha miongoni mwa wengine.
Mechi nyingine ya Eufa itakuwa baina ya Fc Porto na Roma ugani Estadio do Drangao nyumbani kwa Fc Porto.
Mechi zote mbili zitaanza mnamo saa tano kamili za usiku.
Comments
Post a Comment