KOGALO WAIBIWA!!!
Timu ya Gor mahia amaarufu kama Kogalo pamoja na mashabiki wanalalamika kuibiwa bao siku
ya jumapili walipokuwa wanacheza kwenye mkondo wa pili dhidi ya NA
Hussein Dey kwenye kikundi chao kwa mechi za kung'ang'ania bingwa
barani Africa CAF.
Kogalo wanasema
walinyang'anywa bao mnamo dakika ya 59 baada ya defenda Shafiq Butambuze
kufunga kwa kichwa chake kutoka kwa krosi iliyopigwa na Francis Kahata.
Mwamuzi
wa mechi hiyo kutoka mali aliamua kuwa mlinda lango wa Hussein Dey
alichezewa visivyo iilhali pich za video zinaonyesha kweli kuwa mlinda
langu huyo alijingoga na mchezaji wake mwenyewe huko wakijaribu
kuondosha hatari.
Uamuzi huo ulilazimisha kogalo kurudi nyumbani bila pointi.
Gor
mahia wamesukumwa hadi nafasi ya pili na pointi sita baada ya kushindwa
hivyo ni lazima wajitahidi kushinda ugenini dhidi ya Zamalek ya Egypt
kabla ya kuaiandaa
Petro Atletico mnamo tarehe 17 mechi.
Gor mahia wanaitaji kumaliza miongoni mwa timu mbili bora katika kundi hilo la D ili kujipa tiketi kwenye robo fainali.
Comments
Post a Comment