Mahakamani

wanaume wawili kwa majina Francis Otieno Ogello na Elijah Okumu Owiti, wameshtakiwa kwenye mahakama ya Winam jijini Kisumu kwa kosa la kumpiga mwanada  Valary Barasa .
Mbele ya hakimu Jackline Mitei, mahakama iliambiwa kuwa washtakiwa pamoja na wengine ambao hawakufika kotini walimpiga na kumuumiza Valary  mnamo tarehe20 mwezi February mwaka huu kwenye eneo la chemelil kaunti ya kisumu.
washtakiwa walikanusha mashtaka.
Kesi hiyo itatajwa tarehe moja mwezi wa nne, mwaka huu.
Kesi zingine zilizokuwa mbele ya mahakama ni pamoja na;
Kesi inayomkabili Erick Nyamongo Nyamache anayetuhumiwa kuibia Charles Otieno Oluoch bidhaa za thamani ya alfu 13 mnamo tarehe 6 mwezi wa saba mwaka jana mtaani Nyamasaria. 
Kesi inayomkabili Eliakim Mwalu anayetuhumiwa kumwibia Faith Kalacia simu aina ya samsung yenye thamani ya alfu kumi na tatu na mia tano mnamo tarehe 28 mwezi february mtaani Mamboleo jijini Kisumu.
Kesi inayomkabili David Oruko Otieno anayetuhumiwa kumpiga na kumuumiza Christine Adhiambo mnamo tarehe nne january mwakani kwenye eneo la Rapogi iliyoko kaunti ya kisumu.
Kesi inayomkabili Peter Oduor Owiti anayetuhumiwa kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka kumi na mbili mnamo tarehe 13 mwezi huu.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals