Mazingira safi

Serikali ya kaunti ya kisumu chini ya idara ya mazingira imeungana leo na wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini kisumu na shirika la exclusive modeling agency ili kusafisha mazingira.

Shughuli hiyo ilifanywa katika soko la kibuye ambapo vijana hao waliungana pia na shirika la CBO,KIWAN na KIKOMOC  kutoa takataka kwenye soko hilo iliyoko kwenye wadi ya kaloleni.

Wakiongozwa na Vincent Ochieng' kutoka kikundi cha exclusive modeling agencies ,walimu na wanafunzzi kutoka vyuo vikuu vilivyo katika kaunti ya kisumu waliungana pamoja kusafisha soko hilo la kibuye.

Meneja mkurugenzi idara ya mazingira ya kaunti ya Kisumu Kenneth Oyoo amesema kwamba mazingira safi ni muhimu sana kwa jamii hivyo basi wakazi wa kisumu wanapaswa kuzingatia usafi wa mazingira.

Bwana Oyoo ameongeza kuwa ,kutakuwa na shughuli hiyo itakuwa inatekelezwa ijumaa ya pili kila mwezi.

vilevile bwana oyoo amewaimiza wananchi kupanda miti.tunapokaribia kuadhimisha siku ya misitu ulimwenguni mnamo tarehe 21 mwezi huu.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals