''Hamstahili Kuvaa Sare Ya Argentina''Maradona Asema
Mchezaji bingwa wa kitambo wa Argetina Diego Maradona amesema kwamba kikosi cha Argentina ya mwaka huu ni bure kabisa na hawastahili kuvaa sare ya timu hiyo.
Hii ni baada ya Argentina kushindwa kwa mabao matatu kwa moja na timu ya Venuzuela kwenye mechi ya kirafiki siku ya jumapili.
Maradona ambaye alishinda kombe la dunia na Argentina mwaka wa 1986 amesema kwamba kikosi hicho cha mwaka 2019 inaleta aibu sana kwa nchi ya Argentina.
Kumbuka Argentina walifika kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil lakini mwaka nne baadaye walilazimishwa kuuaga mashindano hayo kwa raundi ya kumi na sita nchini Russia.
Juhudi zake Lionel Messsi za kuishindia timu yake ya taifa angalau kombe zimegonga mwamba hata baada ya kurudi kutoka kustaafu kwenye mechi za kimataifa.
Alipoulizwa kaa alitazama mechi hiyo,Maradona alijibu kwa kejeli na kusema ''sipendi kutazama filamu za kutisha ila sielewi ni kwa nini wasimamizi wa Argentina walidhani watapata ushindi dhidi ya Venuzuela.''
Maradona ambaye alikuwa pia kocha wa kitambo wa Argentina aliongeza kwa kumlaumu rais wa mpira nchi hiyo { Argentinean Football Association} Claudio Tapia,na kudai kwamba ameshindwa kufanya kazi.
Vilevile ,Maradona amesema kwamba mashabiki pamoja na wachezaji waache kupatia nahodha wao Mesii shinikizo nyingi sana kwa kuwa hawezi cheza peke yake.
Kumbuka Messi atakosa mechi inayofuata ya kirafiki dhidi ya cameroon baada ya kupata majeraha.
Hii ni baada ya Argentina kushindwa kwa mabao matatu kwa moja na timu ya Venuzuela kwenye mechi ya kirafiki siku ya jumapili.

Kumbuka Argentina walifika kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil lakini mwaka nne baadaye walilazimishwa kuuaga mashindano hayo kwa raundi ya kumi na sita nchini Russia.
Juhudi zake Lionel Messsi za kuishindia timu yake ya taifa angalau kombe zimegonga mwamba hata baada ya kurudi kutoka kustaafu kwenye mechi za kimataifa.
Alipoulizwa kaa alitazama mechi hiyo,Maradona alijibu kwa kejeli na kusema ''sipendi kutazama filamu za kutisha ila sielewi ni kwa nini wasimamizi wa Argentina walidhani watapata ushindi dhidi ya Venuzuela.''
Maradona ambaye alikuwa pia kocha wa kitambo wa Argentina aliongeza kwa kumlaumu rais wa mpira nchi hiyo { Argentinean Football Association} Claudio Tapia,na kudai kwamba ameshindwa kufanya kazi.
Vilevile ,Maradona amesema kwamba mashabiki pamoja na wachezaji waache kupatia nahodha wao Mesii shinikizo nyingi sana kwa kuwa hawezi cheza peke yake.
Kumbuka Messi atakosa mechi inayofuata ya kirafiki dhidi ya cameroon baada ya kupata majeraha.
Comments
Post a Comment