Watutu wafariki kwenye ajali Mamboleo!
Watu watatu wamefariki papo hapo, baada ya lori la Kampuni ya Coca Cola kumgonga muhudumu wa pikipiki na kisha kugonga tuk tuk katika eneo la Mamboleo Junction jijini Kisumu.
Lori hilo lililokua limebeba chupa za soda, lilikua safarini kutoka upande wa Kakamega kuja hapa Kisumu kabla ya ajali hiyo.
Inadaiwa kua breki za gari hilo zilifeli kabla ya kumgonga muhudumu wa boda boda aliyefariki papo hapo, na kisha kuigonga tuk tuk iliyokua na mume, mke na mwanao wa takribani miaka mitatu.
Mama na mtoto waliaga dunia papo hapo, huku mume ambaye alikua dereva wa tuk tuk hiyo akijeruhiwa. Dereva wa lori hilo pia alijeruhiwa.
Wawili hao walipelekwa kupokea matibabu kwenye Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga almaarufu Russia, huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitalini humo.
Wakaazi wa eneo hilo wametaka matuta ya barabarani kuwekwa barabarani ili kupunguza mwendo wa magari, pikipiki na tuk tuk kama njia moja ya kudhibiti visa vya ajali.
Lori hilo lililokua limebeba chupa za soda, lilikua safarini kutoka upande wa Kakamega kuja hapa Kisumu kabla ya ajali hiyo.

Mama na mtoto waliaga dunia papo hapo, huku mume ambaye alikua dereva wa tuk tuk hiyo akijeruhiwa. Dereva wa lori hilo pia alijeruhiwa.
Wawili hao walipelekwa kupokea matibabu kwenye Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga almaarufu Russia, huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitalini humo.
Wakaazi wa eneo hilo wametaka matuta ya barabarani kuwekwa barabarani ili kupunguza mwendo wa magari, pikipiki na tuk tuk kama njia moja ya kudhibiti visa vya ajali.
Comments
Post a Comment