Mwanamme mmoja kwa jina Erick Omondi ameshtakiwa kwenye mahakama ya Winam jijini Kisumu kwa tuhuma ya wizi.
Mbele ya hakimu Jackline Mitei, mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa pamoja na wengine ambao hawakufika kotini walivunja maktaba na kuiba vitabu pamoja na vitu vingine enye thamani ya shillingi alfu 48200 mnamo tarehe 13 mwezi wa Agosti mwaka jana kwenye shule ya sekondari ya wasichana st.Ignatious Loyola iliyoko manyatta kaunti ya kisumu.
mshtakiwa alikanusha mashtaka.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 26 mwezi Aprili, mwaka huu.
Vilevile,mahakama
hiyo imetupilia mbali kesi inayomkabili Philip Nyadero anayetuhumiwa kuibia
kampuni ya Kinagor dairy vitu vya thamani ya shilingi alfu 140000.
Mbele ya
hakimu Jackline Mitei, Mahakama iliambiwa kuwa baada ya kuchunguza vizuri
kampuni ya kinagor imepata kwamba bwana Philip hana hatia kwa hivyo waliomba
mahakama kumwachilia.
Bwana
Philip Nyadero aliachiliwa huru.
Comments
Post a Comment