Kilio Cha Vijana Wanaoranda Randa Mtaani
Vijana wanaorandaranda mtaani almaarufu kama Chokora hupitia
mashida mengi sana wanapozurura kando ya barabara zetu mtaani.
Kumbuka kila kitendo chema sadaka,kwa hivyo ukiwa na uwezo vijana hawa wanakuitaji.
Vijana hao hujipata wakiranda randa mtaani kwa sababu mbalimbali,zikiwa pamoja na;
Kutoroka nyumbani kwa sababu ya umaskini,mateso na pia dhuluma ya kimapenzi ,kuzaliwa kwenye maisha hayo,Kuachwa na kutupuliwa na wazazi wao,kutaka tu kukaa kwenye jiji na pia jamii kutojali.
Vijana hawa hupitia changamoto nyingi sana kama vile,kutusiwa,kupigwa,kutumia miadarati,kunajisiwa,njaa,mimba zisizotarajiwa na kukaa kwenye mazingira duni.
Nilipozungumza na baadhi ya vijana waliokuwa mitaani ya
Ondiek iliyoko jijini Kisumu,vijana hao walianiarifu kuwa changamoto yao kubwa
ni kukosa chakula,kukosa mahali pa kulala na pia kupuuziwa kuwa wezi.
Vilevile vijana hawa waliomba serikali iwasaidia
kwa njia yeyote kwa kuwapa nafasi za kazi na pia mtu yeyote anayeweza
kuwasaidia kwa njia yeyote ile askie kilio chao.
Kumbuka kila kitendo chema sadaka,kwa hivyo ukiwa na uwezo vijana hawa wanakuitaji.
Comments
Post a Comment