Ligi Kuu Nchini

Mechi kadhaa za ligi kuu ya soka nchini-kpl,zimechezwa hivi leo kwenye uga tofauti kote nchini.

Mabingwa wa ligi mara kumi na saba Gor mahia almaarufu kogalo wameilaza Zoo Kericho kwa mabao manne kwa sufuri kwenye mechi iliyoandaliwa ugani Green stadium Kericho.
Nahodha Denis Oliech alicheka na wavu mara mbili mtawalia kabla  ya Kenneth Mugana na Nicolas kipkirui kujiandikisha katika kitabu cha wafunga bao.
 
Matokeo mengine ni kama yafuatayo;
 
Timu ya sofapaka imeshinda mt.Kenya kwa mabao tatu kwa moja ugani Kenyatta.

Kakamega homeboyz wamepiga Bandari fc kwa mabao mawili kwa moja ugani Mbarika sports club.

Tusker fc wameshinda Kariobangi Sharks kwa mabao tatu kwa moja ugani ruaraka.

Huko Ulinzi stars wakiilaza Sony sugar kwa mabao mawili kwa moja ugani Afraha.

 Vihiga united wametoka sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya FC leopards ugani Bhukungu.

 KCB wakitesa nyasi bure dhidi ya Western Stima na kutoka na sare ya bao moja kwa moja ugani Nairobi City Stadium.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals