zilizotokea mahakamani
Mahakama
ya Winam jijini Kisumu, imeahirisha kesi inayomkabili Fredrick Odhiambo
anayetuhumiwa kwa kesi mbili kujifanya polisi na pia kumiliki madawa za
kulevya.
Mbele
ya hakimu Benard Kasavuli, mahakama iliambiwa kua bwana Ezekiel
alipatikana mnamo tarehe ishirini mwezi huu maeneo ya kondele iliyoko
kisumu akiwa na bhangi 'roals' tatu na uko akijifanya kuwa polisi.
Fredrick alikanusha mashtaka hayo, na kuomba kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 50 pesa taslimu, au shilingi alfu 10 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 6 mwezi ujao mwaka huu.
Comments
Post a Comment