Timu ya Atletico Madrid ilicharaza vijana wa Juventus kwa mabao mawili kwa sufuri kwenye mkondo wa kwanza za mechi za raundi ya kumi na sita ya kombe la Eufa.Mechi hiyo ilichezwa usiku wa jumanne kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano nyumbani kwa Atletico madrid.
Atletico walipata bao lao la kwanza kupitia kwa defender wao Jose Gimenez mnamo dakika ya 78 kabla ya Diego Godin kuongeza la pili dakika tano baadaye.
Juhudi zake mchezaji bingwa Christiano Ronaldo kupatia timu yake ushindi iligonga mwamba na hata za mwenzake mpotugali Diblo Dyballa pia hayakufua dafu uko wakishindwa na Vijana wa Diego Simeon.
Kwingineko,Vijana wa Pep Guardiola Manchester City walishinda Schalke 04 kwa mabao matatu kwa mawili ugenini  Veltins Arena kwa wanaSchalke04.
Manchester city ndiye waliotangulia kufunga mnamo dakika ya 18 kupitia kwa mchezaji Sergio Kun Aguero lakini wanaSchalke 04 walijibu kwa mpigo kwa mabao mawili mnamo dakika ya 38 na 45 mtawaliwa,bao zote za schalke zilifungwa kupitia kwa kituta cha penalti na mchezaji Nabil Bentaleb baada ya wanamancity kucheza visivyo.
Mambo yalianza kuenda segemnenge kwa vijana wa pep baada ya Nicolas Otamendi kuonyeshwa kadi nyekundu mnamo dakika ya 68 lakini walipata nafuu dakika ya 85 ambapo Lorey sane alifunga bao la pili na kusawazisha mambo kabla ya Raheem Sterling kufunga bao la ushindi dakika ya 90.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals