mwanaume ashtakiwa mahakamani na kosa la kunajisi msichana

Mwanaume mmoja anayefahamika kama Erick Odhiambo amefikishwa mbele ya mahakama ya Winam jijini Kisumu .Erick anatuhumiwa kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka kumi na saba.
Mbele ya hakimu Fatuma Mwanza Rashid, mahakama iliambiwa kua bwana Erick alifanya kitendo hicho mnamo tarehe 20 mwezi huu wa February kwenye mtaa wa mamboleo iliyoko kisumu.
Erick alikanusha mashtaka hayo, na kuomba kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 125 pesa taslimu, au shilingi alfu 250 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 9 mwezi Mei, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals