mchezoni
Ligi kuu nchini KPL itarejea leo kwa mechi moja ambapo Gor Mahia
almaarufu kama Kogalo wataandaa vijana wa western stima kwenye uga wa
Moi International Sports Centre,Kasarani.Mechi hiyo itachezwa saa kumi
alasiri.Kumbuka Kogalo wako nafasi ya tatu kwenye jedwali ya ligi wakiwa
na alama 25 baada ya kucheza mechi 12{mechi moja nyuma ya viongozi
Bandari ambao wako na alama 28},Western Stima nao wako nafasi ya 7 na
alama 20.
Kwingineko mechi za kombe la Eufa ziliendelea
usiku wa juma nne kwa mechi mbili tofauti.Barcelona walilazimishwa
kutoka sare bila bao lolote ugenini kwa Olympique Lyonnais,juhudi zake
mchezaji bingwa Lionel Messi kupatia timu yake bao iligonga mwamba na
kuwalazimisha kugawa alama.
Liverpool pia walitesa nyasi bure ugani Anfield walipoandaa Bayern Munchen.
Mechi
zingine zitaendelea leo usiku ambapo Atletico Madrid wataandaa
Juventus,vilevile Fc Schalke 04 watakaribisha vijana wa Manchester
city.Mechi zote zitachezwa kuanzia saa tano.
Comments
Post a Comment