LIGI KUU NCHINI,KPL
Mechi za KPL ziliendelea jana kwenye
uga tofauti nchini.
Mechi izo ziling'oa nanga mnamo
saa nane mchana na mchuano kati ya KCB Fc na Vijana wa Sony sugar kwenye uga wa Kenyatta stadium Machakos ambapo vijana wa KCB walishinda kwa bao moja kwa sufuri.Mechi zingine zilikuwa pamoja na ya Zoo Kericho wakichuana na mathare united kwenye uga wa green stadium Kericho mechi iliyoisha sare ya kutokuwa na bao lolote.
kwingineko posta rangers walishinda vihiga united kwa bao moja kwa sufuri kule mumias sports complex ilioko mumias.Western stima nao pia walichapa vijana wa mount kenya kwa mabao mawili kwa moja kule moi stadium kisumu.
Vilevile Ulinzi stars walicharaza AFC Leopards kwa bao moja kwa sufuri mechi iliyochezwa kule Kenyatta stadium machakos.
Shughuli hayo hayakuisha kabla ya vijana wa Gor mahia almaarufu kama Kogalo kulaza sofapaka kwa bao moja kwa sufuri kwenye mechi ya kukata na shoka iliyochezwa kwenye uga wa Moi International sports centre Nairobi.
Kumbuka Bandari Fc ndiye wanaongoza kwenye jedwali ya ligi kuu ya kpl wakiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi kumi na tatu,Madhare united wanafuata kwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 26 baada ya kucheza kumi na nne,Gor Mahia wanafunga tatu bora wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi kumi na mbili.
Mechi za kpl zitarejelea kaitkati ya wiki mnamo siku ya juma tano ambapo mechi mbalimbali zitachezwa .
Comments
Post a Comment