Mahakamani

Mahakama ya Winam jijini Kisumu, imeahirisha kesi inayomkabili Collince Otieno Ogello anayetuhumiwa kupokea pesa kwa njia za udanganyifu.
Mbele ya hakimu Joseline Mutehi, mahakama iliambiwa kua mwanamme huyo alipokea pesa kutoka kwa Benard Oyalla, akidai kua yeye ni ajenti wa Eldama comfort house iliyoko mtaani Bandani jijini Kisumu.
Benard amesema kuwa alimpa Collince shilingi 10,000 akiahidi kuwapa huduma za Eldama comfort house.
Collince Otieno alikanusha mashtaka hayo, na kuomba kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 5 pesa taslimu.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 9 mwezi April, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals