kesi mahakamani
Mahakama ya Winam jijini Kisumu, imeahirisha
kesi inayomkabili Ezekiel Nyambane anayetuhumiwa kufanya biashara bila leseni .
Mbele
ya hakimu Benard Kasavuli, mahakama
iliambiwa kua bwana Ezekiel alipatikana mnamo tarehe kumi na nane mwezi
huu akiuza madawa kwenye duka la dawa moja liitwalo kama Ziwa iliyoko
kisumu.
Ezekiel alikanusha mashtaka hayo, na kuomba
kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 10 pesa taslimu, au shilingi alfu 20 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 18 mwezi Juni,
mwaka huu.
Comments
Post a Comment