Mwanamme
mmoja kwa jina Baraka Churchil Otieno , ameshtakiwa kwenye mahakama ya
Winam jijini Kisumu kwa kumnajisi msichana mwenye umri wa miaka 11.
Mbele
ya hakimu Benard Kasavuli, mahakama iliambiwa kua mshtakiwa alitekeleza
uhalifu huo tarehe 19 mwezi huu, mtaani Obwola jijini kisumu.
Mshtakiwa alikanusha mashtaka, na kuomba kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 100 pesa taslimu, au shilingi alfu 200 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 11 mwezi Machi, mwaka huu.
Comments
Post a Comment