Mahakamani:wanawake taabani


 Mahakama ya Winam jijini Kisumu, imeahirisha kesi inayomkabili Fiona Awino anayetuhumiwa kuumwibia mwajiri wake kwa jina la purity Anyango .


Mbele ya hakimu Fatuma Mwanza Rashid, mahakama iliambiwa kua mwanadada huyo alimwibia mdozi wake pesa takriban elfu hamsini na nane na mia sita mnamo juma mosi tarehe kumi na sita mwakani uko mtaa wa car wash iliyoko kisumu.
Fiona alikanusha mashtaka hayo, na kuomba kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 50 pesa taslimu, au shilingi laki moja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 8 mwezi Aprili, mwaka huu.
Tukisalia mahakamani,Samantha Atieno alikubali mashtaka baada ya kuhutumiwa kuuza pombe bila leseni kwenye mtaa wa molem ilioko jijini kisumu.Alitozwa faini ya alfu ishirini ama mwezi sita gerezani.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals