Mchuano za KPL

Mechi za kung'ang'ania kombe la KPL zitaendelea wikendi hii kwenye uga tofauti nchini.Kumbuka Mathare united ndiye bado wanaongoza kwenye jedwali ya kombe hilo.
 Mechi izo zitang'oa nanga kesho mnamo saa nane mchana na mchuano kati ya Mount Kenya United Fc na Viongozi wa jedwali Mathare united kwenye uga wa Nyayo jijini nairobi.Kisha posta rangers watajibwaga ugani kipchoge keino stadium kuchuana na Tusker fc mnamo saa tisa jioni.Vilevile Ulinzi stars watacheza na  chemelil ugan Afraha iliyoko nakuru mnamo saa kumi na robo.
Mech zingine zote zitaendelea siku ya jumapili saa tisa jioni zikiwemo Kakamega homeboyz dhidi ya Vihiga united kwenye uga wa Afrah.Nzoia sugar pia watacheza dhidi ya Sony Sugar kwenye uga wa Masinde Muliro iliyoko Bungoma .
Vilevile Mabingwa wa kombe la sportpesa kariobangi Sharks pia wataendeleza kampeni  zao dhidi ya sofapaka fc ugani Nairobi city stadium.Vijana wa Zoo kericho pia watamenyana na Kenya Commercial Bank ugani Green stadium Kericho.
Kisha Bandari fc watamaliza shughuli izo kwa kualika Fc Leopards kwenye uga wa Mombasa stadium .

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals