Waaguzi watisha kugoma

Kuna hofu baina ya wakazi wa kisumu hasa jamaa na marafiki za wagonjwa katika mahospitali mbalimbali za uma.Hii wasiwasi inakuja baada ya shirikisho linalosimamia waaguzi kuonya kuwa wataenda mgomo mnamo Juma tatu tarehe nne mwezi huu.Waaguzi hao wanadai kuwa serikali haijatimiza makubaliano yao ya kuwapa marupurupu mbalimbali na kupandishwa cheo kutokana na maelewano kati yao mnamo November 2011.
Tulipozungumza na mkurugenzi mkuu wa Afya wa Kisumu county bwana Stephene Otieno Sewe alisema bado wanafanya juhudi zote kuhakikisha kwamba matakwa ya waaguzi hao yametatuliwa.
Tukisalia kwa habari za afya,wakazi wa kisumu bado wanajitokeza kwa sehemu tofauti ya kaunti ili kusajiliwa na uhc.Kumbuka shughuli hiyo ya kusajili watu ilifaa kukamilisha jana tarehe 31 lakini imesukumwa mbele hadi tarehe 23 mwezi huu ili kupatia muda wale ambao hawajajisajili kuja kujiandikisha .
Mkurugenzi mkuu wa afya,kisumu kaunti Bwana Stephene Otieno Sewe ameimiza wakazi wa kisumu kujitokeza kijiandikisha na huduma ya afya ya kupatiana matibabu ya bure almaarufu kama UHC.Amesema kwa sasa hivi watu takriban 650,000 tayari wamejiandikisha na uhc hivyo basi inabakisha watu karibu 550,000 ambao hawajajisajili,kumbuka kisumu kaunti iko na watu takriban milioni moja nukta mbili.
Vilevile bwana Sewe amesema kwamba wameheka mikakati mbalimbali,zikiwa pamoja na kutuma ajenti kwa shuleni mbalimbali ili kupata takwimu yao ikilanganishwa na ya wazazi,kutuma ajenti kwa hospitali mbalimbali na pia kuna wale watu wa afya wanaojitolea kutoka kwa jamii kuhakikisha kwamba hakuna mwananchi anakosa kusajiliwa na uhc.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals