Kogalo watishwa
Kocha ya timu ya Hussein Dey kutoka Algeria ametisha kuonyesha Gor mahia
madharau walionyeshwa Nairobi kabla ya mechi yao siku ya juma pili
waliopoteza kwa mabao mawili kwa sufuri.


Kocha huyo
anadai kuwa hawakupewa basi na hata walifanya mazoezi kwenye uga ya
kucheza kriketi kisha wakatupiwa vitu kwa uwanja walipokuwa
wakichuana.
Kocha huyo ameahidi wanakogalo kuwa pia wao watafanyiwa vivyo hivyo wanapoenda ugenini kule Algeria wikendi.
Amepeleka malalamishi kwa tume ya kusimamia mpira Africa CAF na pia wasimamizi wa mechi hiyo.
Kogalo nao wamesema hawaogopi chochote wanapojiandaa kumenyaana siku ya juma mosi kule Algerias na liwe liwalo.
Comments
Post a Comment