Sarri Apata Afueni Baada Ya Ushindi Ya Chelsea Dhidi Ya Totenham

Sarri alifanya badiliko moja kuu ambapo alimwacha mlinda lango Kepa Arrizabalaga nje na kuchezesha Willy Cabalero,hii ni kufuatia tukio lillilotokea siku ya jumapili ambapo Kepa alikataa kufanyiwa mabadiliko kwenye mechi dhidi ya Manchester City baada ya kupata majeraha.
Kitendo hicho kilionyesha kukosa heshima kwa mkufunzi na hata kusababisha kushindwa kwenye matuta za penalti na timu ya Manchester city.
Sarri aliamua kumwadhibu kwa kutomchezesha.Aidha mkufunzi huyo amesema kuwa hataki kumwaribia mchezaji huyo kazi kwa hivyo atamchezesha kwa mechi zijazo.Kepa vilevile ametozwa faini ya kutolipwa wiki moja .
Chelsea walionyesha mchezo mzuri waliposhinda vijana wa Totenham kwa mabao mawili kwa sufuri .Pedro Rodriguez ndiye aliyetangulia kufanga kabla ya Kieran Trippier kujifungia kwenye lango lake baada ya kutoelewana na mlinda lango Lorris.
Kwingineko, timu ya Liverpool walichapa vijana wa Watford kwa mabao 5 kwa sufuri.Sadio mane alifunga mara mbili kabla ya Divok Origi kuheka lake kishaVirgil van Dijk kumalizia na zake mawili.Ushindi huo umeheka Liverpool kwa nafasi ya kwanza wakiwa na alama 69 baada ya kucheza mechi 20.
Matokea za mechi zingine za epl ni pamoja na;
Mancity walishinda vijana wa Westham United kwa bao moja kwa sufuri bao lilifungwa kupitia tuta la penalti na mchezaji Sergio Kun Aguero.
Arsenal waliadhibu Bournemouth kwa mabao 5 kwa moja huko Manchester United wakishinda Crystal Palace kwa mabao 3 kwa moja.
kwingineko nchini Uhispania,Barcelona walishida Real Madrid kwa mabao tatu kwa sufuri na kuwabandua kwenye kombe la Copa Del Rey.Mchezaji bingwa wa Uruguay Luiz Suarez alicheka na wavu mara mbili kabla ya kulazimisha kiungo cha nyuma wa Real madrid kujifanga kwenye goli lake.
Comments
Post a Comment