Sarri taabani

 Timu ya Chelsea hawakutuzwa kwao Stamford Bridge walipolazwa mabao mawili kwa sufuri na timu ya Manchester United kwenye mechi ya raundi ya tano ya kipute cha FA jana usiku.Hivyo basi chelsea  wamebanduliwa kutoka kwa mashindano hayo.
Matokeo hayo yanauweka uongozi wa mkufunzi wa Chelsea Sarri katika hali mbaya,huko united ikijibu baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza chini ya ukufunzi wa Ole Gunna Soljkskjear na kujinyakulia nafasi kwenye robo fainali dhidi ya Wolvehampton.
Ander Herrera alifunga bao la kwanza baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwa Paul Pogba mnamo dakika ya 31 kabla ya Pogba kuongeza bao la pili kupitia kichwa dakika chache kabla ya mapumzikoni.
Tukisalia mchezoni,Liverpool itaiandaa Bayern Munchen kwenye mechi ya kikundi cha Eufa leo usiku.
Mechi hiyo itachezwa ugani Anfield kuanzia saa tano za usiku.
Vilevile Timu ya Barceleona itakuwa ugenini dhidi ya Olympique Lyonnais kwenye kampenzi za kombe hilo la Eufa,

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals