Mlinda Lango Wa Chelsea,Kepa Alaumiwa Kufuatia Kichapo Cha Man City
Timu ya Chelsea ilionyesha mchezo mzuri kwenye fainali za kombe la carabao dhidi ya Manchester City iliochezwa jumapili usiku kabla ya mlinda langu wao Arrizabalaga Kepa kudinda kubadilishwa Timu zote zilikuwa sare ya kutokuwa na bao na ilikuwa dhahiri shairi kuwa mshindi angejulikana kwa matuta za penalti.
Mlinda langu wa akiba Willy Cabalero alikuwa tayari kuingia baada ya Kepa kupata majeraha lakini mlinda langu huyo akasema ako sawa na kunyima Cabelero 'ambaye ana ujuzi sana kwa kushika matuta za penalti nafasi ya kuokoa ''The Blues'.
Kitendo hicho kilikasirisha sana Maurio Sarri ambaye ako kwa hali mbaya sana na uhenda akapoteza kazi yake.Sarri alisema kwamba atazungumza na Kepa ili kujua shida kubwa linaeza kuwa wapi.
Mchezaji Eden Hazard na Ngolo Kante walionyesha mchezo mzuri na hivyo kupatia mashabiki matumaini kuwa chelsea wangeshinda mechi hiyo na kupunguza aibu baada ya kushindwa 6-0 na man city lakini mambo haayakuenda vizuri kwa wanachelsea waliposhindwa kwa mabao manne kwa tatu kwenye matuta za penalti baada ya David Luiz na Jorginho kupoteza matuta zao mtawaliwa.
Chelsea watachuana na timu ya Totenham siku ya juma tano kwenye kombe la EPL.
Comments
Post a Comment