Jumbe za rambirambi kwa mwana-mziki Kantai

Wakenya mbalimbali wanazidi kutuma ujumbe za rambi rambi kwa jamaa,marafiki na familia ya Marehemu mwana-mziki Chris Kantai. Kantai alifariki siku ya jumatano asubuhi kwenye hospitali ya St.Francis jijini Nairobi ambapo amekuwa akilazwa kuanzia jumatatu baada ya kuanza kuuguwa. Kupitia ujumbe kutoka kwa mwakilishi wa familia Wanjiku Thuku,amesema kwamba Chis Kantai ambaye anayefaamika sana kwa nyimbo zake zilizovuma kama Huu Ni Nani,Ting' Badi Malo akimshirikisha Khaligraph Jones na hata Happy wakiimba na mwanadada STL,alikufa baada ya kuwa na shida ya kupumua. Ameongeza kwamba mipango za kuandaa mazishi zinaenedelea na atazidi kueleza mashabiki na marafiki siku ya kumzika mwenda zake Chris. Kantai ameecha nyuma bibi na mtoto mmoja.Atakumbukwa kwa nyimbo zake mbalimbali zilizovuma na pia itakumbukwa kuwa Kantai ndiye aliyeleta mwana-mziki bingwa Stella mwangi kwenye miziki na ngoma yao ya Happy. Amefariki akiwa na umri wa miaka 42. Wanamziki mbalimbali wametoa ...