Posts

Showing posts from 2019

CAMPUS HOBBIES

Image
‘’All work and no play makes Jack a dull boy’’. Hard work is necessary to achieve our goals in life,however concentration on work alone without setting aside time to relax makes a person dull .The human mind can work for a long time but it also needs time to relax to avoid being overtaxed. Our daily schedule is usually crowded with duties and assignment therefore one need to have time to relax and rechannel their energy for the task to come. Hobbies therefore are those activities we do regularly in our leisure time for pleasure. They depend on what one prefer to be fun and pleasurable in accordance to his/her own field of passion, interest and expertise.people of the same age brackets usually tend to have the same hobbies because of the common interests. There are tons of hobbies around the world but I would like to focus on campus student’s hobbies. Unlike secondary schools and primary schools, university curriculum is quite flexible and gives more time for students to engage ...
Image
Miamba wa soka nchini Gor Mahia wamepanua mwanya wa alama nane kileleni kwa jedwali la ligi kuu ya soka nchini – KPL, kufuatia ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Sony Sugar ugani Moi jijini Kisumu. Sony Sugar walikuwa kifua mbele mara mbili kwenye  mechi hiyo huko Enock Agwanda na Nyatini J wakifungia timu kabla ya Jacquis Tuyisenge na Samwel Onyango kuisawazishia Gor Mahia. Kumbuka Mechi hiyo ilisisimamishwa mara nne baada ya kocha na wachezaji kuzua vugu kutoridhishwa na maumuzi mbalimbali za mwamuzi wa mechi hiyo.  Mlinda lango wa sony Nyau Samwel alionyeshwa kadi nyekundu dakika za mwisho kwenye mechi hiyo huko kocha mkuu wa Sony Patrick Odhiambo pia  akionyeshwa nyekundu kwa kuzozana na mwamuzi. Mabao hayo manne yalifungwa kwenye kipindi cha kwanza huku Nicolas Kipkirui akiifungia Gor Mahia bao la ushindi, dakika ya 80 ya mchezo huo kupitia mkwaju wa penalti. Kocha mkuu wa Gor Mahia Hassan Oktay, ameonyesha kufurahishwa na matokeo hayo na kusema m...

Yaliyotekea Kwenye Ligi Kuu Uingereza

Image
Timu ya Chelsea wameongeza matumaini yao ya kumaliza ligi ligi kuu ya Uingereza kwenye nne bora,hii ni baada ya kutoka nyuma bao moja na kushinda Cardif City kwa mabao mawili kwa moja siku ya jumapili ugani Cardif. Cardif City walipata bao mnamo dakika ya 46  mguu yake Víctor Camarasa lakini Chelsea walijibu bao hiyo kipindi cha pili mnamo dakika ya 84 kupitia kwa nahodha yao Cezar Azpilicueta  kabla ya Rouben Loftus Cheek kuingizwa dakika za ushee na kufunga bao la ushindi kutoka kwa krosi yake Wilian. Mchezaji bingwa raia wa Ubelgiji Eden Hazard alileta matumaini kwa timu ya Chelsea alipoingizwa baada ya timu hiyo kushindwa kupata bao. Ushindi huo imempea Meneja Maurizio Sarri afueni baada ya mashabiki kutaka afutwe kazi . Matokea hiyo pia ina maana kuwa chelsea wako kwenye nafasi ya tano  wakitoshana na Arsenal na pointi 60,huko wakiwa pointi moja nyuma ya Manchester United. Meneja wa Cardif Warnock hakufuraishwa na maamuzi ya bao la Azpilicueta huko a...

Marufuku Kwa Mifuko Sokoni

Image
Hisia mbalimbali zinazidi kutolewa na wananchi kuhusu agizo ya serekali kupitia mamlaka ya utunzi  wa Mazingira NEMA ili kupiga marufuku mifuko vya kubeba bidhaa sokoni almaarufu Uhuru bag.           NEMA inadai kuwa mifuko hizo hazijatimiza kiwango inayotakikana na shirika la kugadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS. Mifuko hizo hazifai kuwa kwenye maduka na soko kuanzia jumapili tarehe 31 mwezi huu.Hivyo basi atakaye patikana nayo atakuwa anakiuka sheria na uhenda akafungwa. Nilipozungumza na baadhi ya wakazi wa Kisumu kwenye soko la Kibuye wamesema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la serikali ,kwa sababu watakosa mifuko vya kuwahekea wateja wao  bidhaa wanaponunua kutoka kwao. Vile vile waliomba serikali ya kaunti kutengeneza vituo vya kutupa taka ili kupunguza uchafuzi wa mazingira kwenye soko zao

Mahakamani

Mahakama ya Winam jijini Kisumu, imeairisha kesi inayomkabili Geofrey Odhiambo anayeshtakiwa kwa kosa la kuiba . Mbele ya hakimu Fatuma Rashid, mahakama iliambiwa kuwa mwanamme huyo pamoja na wengine ambao hawakufiki mbele ya mahakama walimwibia Philip Nyamonga miti za uzio kwa boma pamoja na rolls kumi za nyaya mnamo tarehe 9 disemba mwaka 2018 kwenye eneo la Wath Orengo iliyo kisumu east,kisumu kaunti. Bidhaa zote ni za gharama ya thamani elfu 70000 Geofrey alikanusha mashtaka hayo, na kuomba kuachiliwa huru. Aliachiliwa na kuagizwa kuleta mashaidi wake siku ya kesi hiyo kusikilizwa. Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 23 mwezi Mei, mwaka huu.  Vilevile Mwanamme mmoja kwa jina Peter Omondi ameshtakiwa kwenye hiyo ya Winam jijini Kisumu kwa kosa la kukiuka sheria za barabara. Mbele ya hakimu Fatuma Rashid, mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa alipatikana mnamo tarehe 18 mwezi huu kwenye barabara ya kisumu kakamega akiendesha gari bila leseni,bila sare ya dereva na ...

Zidane Anamtaka Mane kwenye Kikosi Chake

Image
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedin Zidane amesema anamtaka mchezaji wa Liverpool raia wa Senegal Sadio Mane kwenye kikosi chake. Mane ambaye ameonyesha mchezo mzuri msimu huu akifunga mabao 11 tangu mwaka ianze , huko akifunga mabao saba kwa mechi tano zilizopita na pia kufunga mabao za kimataifa dhidi ya Watford kwenye ligi kuu ya Uingereza na Bayern Munich kwenye kombe la klabu bora Eufa. Tangu kocha huyo Mfaransa kurejea Santiago Bernabeu Mane amekuwa akitarajiwa kuungana na timu hiyo kwa kuwa Zidan alikuwa akimtaka sana kabla kujiuzulu msimu uliopita. Mane mwenye umri wa miaka 26 hajaonyesha hisia yeyote ya kujiunga na Madrid. Guillem Balague ambaye ni mtaalam wa soka uhispania amesema kwamba hakuna uwezekano ya Mane kuja Madrid msimu huu.

Ligi Kuu Nchini

Image
Mechi kadhaa za ligi kuu ya soka nchini-kpl,zimechezwa hivi leo kwenye uga tofauti kote nchini. Mabingwa wa ligi mara kumi na saba Gor mahia almaarufu kogalo wameilaza Zoo Kericho kwa mabao manne kwa sufuri kwenye mechi iliyoandaliwa ugani Green stadium Kericho. Nahodha Denis Oliech alicheka na wavu mara mbili mtawalia kabla  ya Kenneth Mugana na Nicolas kipkirui kujiandikisha katika kitabu cha wafunga bao.   Matokeo mengine ni kama yafuatayo;   Timu ya sofapaka imeshinda mt.Kenya kwa mabao tatu kwa moja ugani Kenyatta. Kakamega homeboyz wamepiga Bandari fc kwa mabao mawili kwa moja ugani Mbarika sports club. Tusker fc wameshinda Kariobangi Sharks kwa mabao tatu kwa moja ugani ruaraka. Huko Ulinzi stars wakiilaza Sony sugar kwa mabao mawili kwa moja ugani Afraha.  Vihiga united wametoka sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya FC leopards ugani Bhukungu.  KCB wakitesa nyasi bure dhidi ya Western Stima na kutoka na sare y...

Maazimio ya Kongamano!

Ni takriban wiki moja tangu kongamano la kimataifa kuhusu makazi ya kutosha na gharama ya chini kukamilika. kongomano hilo ambayo ilipangwa na shirika la Grassroot Trust ikiungana na kaunti ya Kisumu ilichukua siku tatu huko watu wakijufunza mambo mengis sana kuhusu makazi bora. Bwana Lawrence Apiyo ambaye ndiye Mratibu wa  Grassroot Trust ameambia radio sahara kwamba kutokana na kongamano hilo ,wako na maazimio mbalimbali za kutekeleza ili  kuimarisha makazi jijini kisumu . Maazimio hayo ni pamoja na; Kuuungana na mashirika zisizo za serikali na serikali ya kaunti ya kisumu ili kuhakikisha kwamba wakazi wa kisumu wanaishi kwa nyumba zenye gharama za chini,zenye usalama na maji,na vituo vya afya. Kuheka mashirika mbalimbali za nyumba na makazi{cooperative housing},kupanga jumuiya wanakoishi wananchi,Kuhekeza ardhi zinazomilikiwa na jamii{community landtrust} na pia kuimarisha sera ya makazi.{housing policy} Bwana Lawrence ameongeza kwamba watatumia mt...
Mwanamme mmoja kwa jina Erick Omondi ameshtakiwa kwenye mahakama ya Winam jijini Kisumu kwa tuhuma ya wizi. Mbele ya hakimu Jackline Mitei, mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa pamoja na wengine ambao hawakufika kotini walivunja maktaba na kuiba vitabu pamoja na vitu vingine enye thamani ya shillingi alfu 48200 mnamo tarehe 13 mwezi wa Agosti mwaka jana kwenye shule ya sekondari ya wasichana st.Ignatious Loyola iliyoko manyatta kaunti ya kisumu. mshtakiwa alikanusha  mashtaka. Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 26 mwezi Aprili, mwaka huu. Vilevile,mahakama hiyo imetupilia mbali kesi inayomkabili Philip Nyadero anayetuhumiwa kuibia kampuni ya Kinagor dairy vitu vya thamani ya shilingi alfu 140000. Mbele ya hakimu Jackline Mitei, Mahakama iliambiwa kuwa baada ya kuchunguza vizuri kampuni ya kinagor imepata kwamba bwana Philip hana hatia kwa hivyo waliomba mahakama kumwachilia. Bwana Philip Nyadero aliachiliwa huru.
If I stay with you, if I'm choosing wrong I don't care at all If I'm losing now, but I'm winning late That's all I want Now we need some space, 'cause I feel for you And I wanna change Growing up alone, it seems so short I can't explain Whatever happens in the future, trust in destiny Don't try to make anything else even when you feel I don't care at all I am lost I don't care at all Lost my time, my life is going on I will be so strong, looking for a new version of myself Cause now all I want is to be a part of my new world Whatever happens in the future, trust in destiny Don't try to make anything else even when you feel I don't care at all I am lost I don't care at all Why not have it all I am lost I don't care at all Lost my time, my life is going on From La casa De papel

''Hamstahili Kuvaa Sare Ya Argentina''Maradona Asema

Image
Mchezaji bingwa wa kitambo wa Argetina Diego Maradona amesema kwamba kikosi cha Argentina ya mwaka huu ni bure kabisa  na hawastahili kuvaa sare ya timu hiyo. Hii ni baada ya Argentina kushindwa kwa mabao matatu kwa moja na timu ya Venuzuela kwenye mechi ya kirafiki siku ya jumapili. Maradona ambaye alishinda kombe la dunia na Argentina mwaka wa 1986 amesema kwamba kikosi hicho cha mwaka 2019 inaleta aibu sana kwa nchi ya Argentina. Kumbuka Argentina walifika kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil lakini mwaka nne baadaye walilazimishwa kuuaga mashindano hayo kwa raundi ya kumi na sita nchini Russia. Juhudi zake Lionel Messsi za kuishindia timu yake ya taifa angalau kombe zimegonga mwamba hata baada ya kurudi kutoka kustaafu kwenye mechi za kimataifa. Alipoulizwa kaa alitazama mechi hiyo,Maradona alijibu kwa kejeli na kusema ''sipendi kutazama filamu za kutisha ila sielewi ni kwa nini wasimamizi wa Argentina walidhani watapata ushindi dhidi ya Venuz...

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Image
Klabu ya Gor Mahia almaarufu kama Kogalo wamekuwa timu ya kwanza nchini kufuzu kwenye robo fainali kwenye mashindano ya kung'ang'ania taji la klabu bingwa Afrika . Kogalo walibaki watu tisa kwenye mechi hiyo baada ya wachezaji wao Ernest Wendo na Shafiq Batambuzi kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi hiyo iliyochezwa ugani kasarani mnamo jumapili. Gor mahia walionyesha umahiri wao kwenye mechi hiyo na kulazimisha timu ya petro Atletico kuenda nyumbani na kubanduliwa kutoka kwa mashindano hayo. Kumbuka Kogalo walihitaji ushindi wowote kwenye mechi hiyo ilinkufuzu huko Petro Atletico wakitaka tu sare yeyote ile .Kwa hivyo ilikuwa mechi ya kukata na shoka huko kila timu ikijaribu kujipea tiketi kwenye robo fainali lakini mwishowe Kogalo ndio waliotoka na ushindi . Kogalo walipata bao yao mnamo dakika ya 56 kupitia mchezaji Jacquis Tuyisenge na mkwaju wa penalti . Kocha wa Kogalo Hassan Oktay alionyeshwa kadi nyekundu na kufukuzwa kando ya uwanja baada ya kukosana na w...

Watutu wafariki kwenye ajali Mamboleo!

Image
Watu watatu wamefariki papo hapo, baada ya lori la Kampuni ya Coca Cola kumgonga muhudumu wa pikipiki na kisha kugonga tuk tuk katika eneo la Mamboleo Junction jijini Kisumu. Lori hilo lililokua limebeba chupa za soda, lilikua safarini kutoka upande wa Kakamega kuja hapa Kisumu kabla ya ajali hiyo. Inadaiwa kua breki za gari hilo zilifeli kabla ya kumgonga muhudumu wa boda boda aliyefariki papo hapo, na kisha kuigonga tuk tuk iliyokua na mume, mke na mwanao wa takribani miaka mitatu. Mama na mtoto waliaga dunia papo hapo, huku mume ambaye alikua dereva wa tuk tuk hiyo akijeruhiwa. Dereva wa lori hilo pia alijeruhiwa. Wawili hao walipelekwa kupokea matibabu kwenye Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga almaarufu Russia, huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitalini humo. Wakaazi wa eneo hilo wametaka matuta ya barabarani kuwekwa barabarani ili kupunguza mwendo wa magari, pikipiki na tuk tuk kama njia moja ya kudhibiti vi...

Taarifa Za Hivi Punde

Image
Draw ya robo fainali kwenye ligi ya mabingwa Eufa imefanywa dakika chache zilizopita. Manchester United watacheza dhidi ya  Barcelona. Juventus dhidi ya Ajax. Huko Liverpool ikichuana na Porto. Manchester City watacheza dhidi ya Totenham. Draw hiyo imeleta maswali mengi kuliko majibu kati ya mashabiki,wachezaji na meneja kote nchini. Maswali hayo ni pamoja na; Je vijana wa Ole Gunner ,Manchester United almaarufu mashetani wekundu wataweza kuzima moto ya Barcelona wakiongozwa na Bingwa Lionel Messi? Je Christiano Ronaldo ataweza kuongoza vijana wa Juventus dhidi ya Ajax ambao walishangaza wengi walipotoa timu ya real madrid ambapo Ronaldo alikuwa akichezea kabla kujiunga na Juventus.

Mahakamani

wanaume wawili kwa majina Francis Otieno Ogello na Elijah Okumu Owiti, wameshtakiwa kwenye mahakama ya Winam jijini Kisumu kwa kosa la kumpiga mwanada  Valary Barasa . Mbele ya hakimu Jackline Mitei, mahakama iliambiwa kuwa washtakiwa pamoja na wengine ambao hawakufika kotini walimpiga na kumuumiza Valary  mnamo tarehe20 mwezi February mwaka huu kwenye eneo la chemelil kaunti ya kisumu. washtakiwa walikanusha mashtaka. Kesi hiyo itatajwa tarehe moja mwezi wa nne, mwaka huu. Kesi zingine zilizokuwa mbele ya mahakama ni pamoja na; Kesi inayomkabili Erick Nyamongo Nyamache anayetuhumiwa kuibia Charles Otieno Oluoch bidhaa za thamani ya alfu 13 mnamo tarehe 6 mwezi wa saba mwaka jana mtaani Nyamasaria.  Kesi inayomkabili Eliakim Mwalu anayetuhumiwa kumwibia Faith Kalacia simu aina ya samsung yenye thamani ya alfu kumi na tatu na mia tano mnamo tarehe 28 mwezi february mtaani Mamboleo jijini Kisumu. Kesi inayomkabili David Oruko Otieno anayetuhumiwa kumpiga...

Kilio Cha Vijana Wanaoranda Randa Mtaani

Image
Vijana wanaorandaranda mtaani almaarufu kama Chokora hupitia mashida mengi sana wanapozurura kando ya barabara zetu mtaani. Vijana hao hujipata wakiranda randa mtaani kwa sababu mbalimbali,zikiwa pamoja na;  Kutoroka nyumbani kwa sababu ya umaskini,mateso na pia dhuluma ya kimapenzi ,kuzaliwa kwenye maisha hayo,Kuachwa na kutupuliwa na wazazi wao,kutaka tu kukaa kwenye jiji na pia jamii kutojali. Vijana hawa hupitia changamoto nyingi sana kama vile,kutusiwa,kupigwa,kutumia miadarati,kunajisiwa,njaa,mimba zisizotarajiwa na kukaa kwenye mazingira duni.                                  Nilipozungumza na baadhi ya vijana waliokuwa mitaani ya Ondiek iliyoko jijini Kisumu,vijana hao walianiarifu kuwa changamoto yao kubwa ni kukosa chakula,kukosa mahali pa kulala na pia kupuuziwa kuwa wezi. Vilevile vijan...