Miamba wa soka nchini Gor Mahia
wamepanua mwanya wa alama nane kileleni kwa jedwali la ligi kuu ya soka nchini –
KPL, kufuatia ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Sony Sugar ugani Moi jijini
Kisumu.
Kumbuka
Mechi hiyo ilisisimamishwa mara nne baada ya kocha na wachezaji kuzua
vugu kutoridhishwa na maumuzi mbalimbali za mwamuzi wa mechi hiyo.
Mlinda
lango wa sony Nyau Samwel alionyeshwa kadi nyekundu dakika za mwisho
kwenye mechi hiyo huko kocha mkuu wa Sony Patrick Odhiambo pia
akionyeshwa nyekundu kwa kuzozana na mwamuzi.
Mabao hayo manne yalifungwa kwenye kipindi cha kwanza huku Nicolas Kipkirui akiifungia Gor Mahia bao la ushindi, dakika ya 80 ya
mchezo huo kupitia mkwaju wa penalti.
Kocha mkuu wa Gor Mahia Hassan Oktay, ameonyesha kufurahishwa na matokeo
hayo na kusema mechi imekuwa ngumu lakini cha muhimu ni kupata pointi zote tatu.
Naye naibu kocha Sony Sugar FC James Odhiambo, ameelezea kuwa Sony sugar wameonewa kwenye mechi hiyo.
Gor
Mahia inaongoza jedwali la KPL kwa alama 45, alama nane mbele ya
nambari mbili Sofapaka. Miamba hao watachuana RS Berkna wa Morocco ugani
Moi Kasarani jijini Nairobi siku ya Jumapili kwwenye mechi ya kung'ania
bingwa barani Africa CAF.
Comments
Post a Comment