Timu ya Kakamega Homeboyz wameshinda vijana wa Bandari Fc kwa mabao
manne kwa sufuri ugani Bukhungu stadium kakamega.Mchezaji Alan Wanga
alicheka na wavu mara mbili alipofunga bao la kwanza na la tatu mnamo
dakika ya 26 na 65 mtawalia.Peter Thiong'o pia alijiheka kwenye kitabu
cha wafunga bao alipoheka bao la pili mnamo dakika ya hamsini na saba
uku Moses Mudavadi akikamilisha shughuli izo alipofunga bao la mwisho
dakika ya themanini na moja.
vilevile Timu ya Zoo Kericho
walifungiwa bao la kipekee kupitia mchezaji Kevin Omondi dhidi ya Fc
Leopards ugani Green stadium ,Kericho.
Kwingineko mabingwawa
kombe la sportpesa Kariobangi sharks walitesa nyasi bure walipotoka sara
ya suluhu bin suluhu dhidi ya viongozi kwenye ligi,Mathare united.Mechi
iliyochezwa Nairobi City stadium.
Tukisalia mchezoni,mabingwa
mara kumi na saba kwenye kombe za KPL Gor mahia wameshinda wapinzani
wao wakali Sony sugar mabao mawili kwa sufuri.Bao zote zilifungwa na
Jaqcuis Tuyisenge mnamo dakika ya 30 na 60 ugani Green stadium Awendo.
Comments
Post a Comment