Hazard aongoza chelsea dhidi ya spurs kuwafikisha fainali za carabao cup

Chelsea wamejinyakulia nafasi kwenye fainali za kombe la carabao dhidi ya Manchester City itakaochezwa ugani wembly  mwezi ujao baada ya kushinda Totenham kwenye mkwajo za penalti jana usiku.
Spurs walikuwa wanaongoza na bao moja kutokana na bao la Harry Kane kwenye mchwano wao wa kwanza,hivyo basi walikuwa wanahitaji tu kutoka sare yeyote ili kuwa kwenye fainali lakini wanachelsea pia walikuwa na nia zingine .
Ngolo kante alitangulia kufunga dakika ya ishirina na saba baada ya kupiga shuti moja kali, kuweka chelsea mbele na kuwa sawa kwa mabao kutokana na mechi ya kwanza kisha baadaye mbelgiji Eden Hazard aliongeza bao la pili dakika kumi baadaye  hivyo basi kutia moyo wanaspurs.
Chelsea ilionyesha mchezo nzuri kwa mechi huo lakini kipindi cha pili ulikuwa wa kusisimua sana baada ya Totenham kusawazisha mambo kupitia kichwa chake Fernando Llorente dakika tano tu baada ya kutoka mapumzikoni.
Kila timu ilijaribu kwa udi na uvumba kupata bao la ushindi lakini juhudi zote ziligonga mwamba kipenga cha mwisho ilipopigwa kuashiria kuwa mechi itaamuliwa kwenye matuta za penalti.
 Mbrazil David Luiz alifunga tuta la kuwafikisha kwenye fainali na kusimamisha kila shabika na wachezaji wa chelsea ugani stamford bridge baada ya Eric Dier na Lucas Moura kupotezea spurs.

Comments

Popular posts from this blog

Mahakamani

Jeshy Tisa Ya Kogalo wabandua Petro Atletico!

Brazil Sent Packing As Croatia Proceeds To Semi Finals