Mahakama ya Winam jijini Kisumu, imeairisha kesi inayomkabili Geofrey Odhiambo anayeshtakiwa kwa kosa la kuiba . Mbele ya hakimu Fatuma Rashid, mahakama iliambiwa kuwa mwanamme huyo pamoja na wengine ambao hawakufiki mbele ya mahakama walimwibia Philip Nyamonga miti za uzio kwa boma pamoja na rolls kumi za nyaya mnamo tarehe 9 disemba mwaka 2018 kwenye eneo la Wath Orengo iliyo kisumu east,kisumu kaunti. Bidhaa zote ni za gharama ya thamani elfu 70000 Geofrey alikanusha mashtaka hayo, na kuomba kuachiliwa huru. Aliachiliwa na kuagizwa kuleta mashaidi wake siku ya kesi hiyo kusikilizwa. Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 23 mwezi Mei, mwaka huu. Vilevile Mwanamme mmoja kwa jina Peter Omondi ameshtakiwa kwenye hiyo ya Winam jijini Kisumu kwa kosa la kukiuka sheria za barabara. Mbele ya hakimu Fatuma Rashid, mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa alipatikana mnamo tarehe 18 mwezi huu kwenye barabara ya kisumu kakamega akiendesha gari bila leseni,bila sare ya dereva na ...
Comments
Post a Comment