Mechi za kpl
Mabingwa mara kumi na saba Gor Mahia almaarufu kama
kogalo ,leo hii watajibwaga ugani ili kuendeleza kampeni zao za kutetea kombe
ilo la KPL kwa mara nyingine dhidi ya timu ya sony sugar kutoka Awendo.
Mechi hiyo itachezwa majira ya saa kumi alasiri kwenye uga ya Afraha jijini Nakuru na siyo machakos kama ilivyopangwa mbeleni.
Sony
sugar ambao ni wapinzani kuu wa Gor Mahia kwa hivi sasa wako mbele ya kogalo uko wakiachana na pointi 1
,vijana wa Awendo wako nambari 8 na point 14 uku kogalo wakiwa nambari 9
na pointi kumi na mbili baaada ya kucheza mechi nane ,mechi moja chini
ya sony sugar.
Tukisalia mchezoni,Timu ya Kariobangi sharks wako bao moja mbele dhidi ya Mathare united kwenye uga wa
Nairobi city stadium,.Kwengineko Kakamega homeboyz bado wanatesa nyasi
bure dhidi ya bandari kule Bhukungu stadium .Vilevile mambo ni sawasawa kati ya Kericho Zoo AFC Leopards uko Grreen stadium,Kericho.
Comments
Post a Comment