kesi mahakama
Mahakama ya Winam jijini Kisumu, imeahirisha
kesi inayomkabili Nancy Awuor anayetuhumiwa kupokea pesa kwa njia za udanganyifu.
Mbele ya hakimu Bernard Kasavuli, mahakama
iliambiwa kua mwanadada huyo alipokea pesa kutoka kwa Dorcas Atieno na Damaris
Atieno, akidai kua angewauzia bidhaa mbali mbali.
Dorcas amesema kuwa alimpa Nancy shilingi 55,000
akiahidi kumuuzia jokovu au friji na runinga.
Damaris naye amesema kua alimpa Nancy
shilingi 25, 000 akiahidi kumuuzia home theatre, mnamo tarehe tisa mwezi wa
Sita mwaka jana.
Nancy Awuor alikanusha mashtaka hayo, na kuomba
kuachiliwa dhamana.
Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 70
pesa taslimu, au shilingi laki mbili na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 14 mwezi Mei,
mwaka huu.
Comments
Post a Comment