kesi mahakamani
Mahakama
ya Winam jijini Kisumu, imeahirisha
kesi inayomkabili Geofrey Omondi Otieno anayeshtakiwa na mashtaka mbili ya kuendesha gari akiwa mlevi na pia kupatiikana na madawa za kulevya
kwenye gari hilo.
Mbele
ya hakimu Bernard Kasavuli, mahakama
iliambiwa kua mwanaume huyo mwenye umri wa kati alipatikana mnamo
tarehe28/01/2019 kwenye njia ya chiga kitu saa tisa unusu ivi akiwa
anaendesha gari akiwa mlevi na pia gari lake kulikuwa na madawa za
kulevya.
Bwana Geofrey alikanusha madai hayo na hivyo basi hakimu akasema angeachiliwa kwa pesa za dhamana za shilingi 100,000.
Kesi hiyo itasikilizwa tarehe28 mwezi Mei,
mwaka huu.
Tukisalia mahakamani Alexandra Orero anayeshatakiwa kuuza pombe baada ya masaa zilizowekwa alikubali mashtaka na kuomba msamaha kwenye koti hiyo ya winam.
Bwana Orero inasemakana kua alikuwa akiuza pombe aina ya trace,napoleon, na bluemoon kondele jijini kisumu mnamo tarehe 28/01/2019 kitu saa tano za mchana.
Ametozwa faini ya shillingi 20,000 ama mwezi tatu gerezani ampewa siku kumi na nne akitaka rufaa.
Comments
Post a Comment