Foleni kwenye usajili ya UHC
Wakazi wa
Kisumu leo hii walijaa kwenye foleni ya kujiandikiza na UHC kwenye sehemu tofauti jijini,wanamatumai kuwa watapokea matibabu za
bure iwapo wataugua hapo mbeleni.UHC ni mojawapo kati ya ajenda nne kubwa za serikali mwaka
huu na kaunti ya kisumu ni moja wapo kati ya zile kaunti nne zikiwemo
Isiolo,Machakos na Nyeri zilizochaguliwa.
Nilipozungumza
na baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa shughuli izo kwenye uga ya
kucheza ya JomoKenyatta,wamesema kuwa wanatumai UHC
itasaidia wananchi wengi sana hasa wasio na uwezo wakujilipia matibabu.
Vilevile Cathy Oduol ambaye ni ajenti ya UHC jijini kisumu pia ameongeza
kuwa mkenya yeyote anaweza jiandikisha na UHC bora awe na kitambulisho na pia
watoto wenye umri kati ya mwaka moja hadi ishirini na tatu wanaweza jiandikisha
pia.
wale
amabao wamejisajili tayari lakini bado wangependa kuongeza watu kwenye
kadi yao wanaimizwa kufanya hicyo kabla ya tarehe thelathini na moja
mwezi huu ambapo shughuli hizo zitaisha.
Comments
Post a Comment