Miamba wa soka nchini Gor Mahia wamepanua mwanya wa alama nane kileleni kwa jedwali la ligi kuu ya soka nchini – KPL, kufuatia ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Sony Sugar ugani Moi jijini Kisumu. Sony Sugar walikuwa kifua mbele mara mbili kwenye mechi hiyo huko Enock Agwanda na Nyatini J wakifungia timu kabla ya Jacquis Tuyisenge na Samwel Onyango kuisawazishia Gor Mahia. Kumbuka Mechi hiyo ilisisimamishwa mara nne baada ya kocha na wachezaji kuzua vugu kutoridhishwa na maumuzi mbalimbali za mwamuzi wa mechi hiyo. Mlinda lango wa sony Nyau Samwel alionyeshwa kadi nyekundu dakika za mwisho kwenye mechi hiyo huko kocha mkuu wa Sony Patrick Odhiambo pia akionyeshwa nyekundu kwa kuzozana na mwamuzi. Mabao hayo manne yalifungwa kwenye kipindi cha kwanza huku Nicolas Kipkirui akiifungia Gor Mahia bao la ushindi, dakika ya 80 ya mchezo huo kupitia mkwaju wa penalti. Kocha mkuu wa Gor Mahia Hassan Oktay, ameonyesha kufurahishwa na matokeo hayo na kusema m...
Posts
Showing posts from April, 2019